Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LHRC wabaini mapungufu sheria ya dhamana nchini

Anna Henga2 Ana Henga, Mkurugenzi Mtendaji LHRC

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na Malalamiko mengikutoka kwa wadau, kuhusu Makosa yasiyokuwa na dhamana na uwepo wa Mlundikano wa mahabusu Magerezani, Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kimeweza kufanya utafiti ili kuangalia kasoro zinazopatikana katika sheria lengo kubwa likiwa kusaidia kuboresha utolewaji wa dhamana.

Kimefikia hatua hiyo ili kuweza kuisaidia jamii kutambua hatua ambazo wanaweza kuzifikia, hasa katika sheria ya dhamana ambayo kwa mujibu wa tafiti hiyo inaonesha kuwa sheria ya Tanzania ina mapungufu katika kipengele hicho.

"Ukiangalia Zanzibar makosa karibia yote yana dhamana, hata malawi, dhamana ni haki, mtu kama bado unatuhumiwa hauna kosa hadi pale Mahakama itakapo thibitisha kuwa una kosa" Ana Henga Mkurungenzi Mtendaji wa LHRC.

Wameeleza kuwa lengo la utafiti huo ni kuangalia ni ainagani ya makosa ambayo hayana dhamana, huku wakioanisha na nchi jirani ili kuweza kupunguza mlundikano wa mahabusu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live