Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

LHRC: Mahakama imuachie mshtakiwa ndani ya siku 60 kama upelelezi haujakamilika

Video Archive
Tue, 11 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya sheria kutaka upelelezi usipokamilika ndani ya siku 60 mshatakiwa kuachiwa huru , jambo hilo halielezwi ipasavyo na mahakama.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Februari 10, 2020 na wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe katika mkutano wa waandishi wa habari kuzungumzia maadhimisho ya siku ya sheria  na mapendekezo ya maboresho ya mifumo ya utoaji haki.

Massawe amesema sheria hiyo ya kumwachia mshatikiwa ipo katika sheria  ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu namba 225(4).

Amesema pamoja na kuwepo kwa sheria hiyo,  mahakama imekuwa haitekelezi, na baadhi ya watuhumiwa wakijikuta wakikaa mahabusu muda mrefu.

"Kuna haja ya wizara ya katiba na sheria kusisitiza utekelezaji katika hili kwani mbali na kuwapa haki watuhumiwa pia itapunguza msongamano wa mahabusu magerezani ambao wanaelezwa kuwa wengi kuliko wafungwa," amesema.

Amesema ni wakati sasa vyombo vinavyowapeleka washatakiwa mahakamani kujidhihirisha katika upelelezi kabla ya kuwafikisha huko na kushauri mahakama iwe na mamlaka ya kufuta shauri husika kama hilo halijatekelezwa.

Pia Soma

Advertisement

Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, Anna Henga ameshauri makosa yote yawe na dhamana kwa kubadilisha masharti ya dhamana kulingana na aina ya kosa jambo litakalosaidia kudumisha dhana ya mtu kutoonekana kuwa na hatia mpaka pale mahakama itakapothibitisha.

"Pia tunaunga mkono kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa siku ya maadhimisho ya sheria kuwa bado kuna changamoto kubwa ya upelelezi wa kesi, jambo linaloashiria kwamba Serikali ipo tayari kuchukua hatua katika kudumisha ustawi wa haki za binadamu hususani katika eneo la mfumo wa utoaji haki," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz