Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kwenye mkesha wa Mwaka mpya jambazi auwawa (+video)

Video Archive
Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Mtu mmoja anayedaiwa kuwa jambazi ameuawa na jeshi la polisi mkoani Kigoma, wakati wa majibizano ya risasi na wenzake watatu kufanikiwa kukimbia wakati wa doria ya mkesha wa mwaka mpya 2021, huku silaha ya kivita aina ya AK47 ikipatikana.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, na kusema kuwa tukio hilo limetokea Desemba 31, 2020, majira ya saa 5:30 usiku, wakati wa mkesha wa mwaka mpya baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wasamalia wema kuwa kuna watu wanatarajia kutekeleza uhalifu hivyo Askari wakafika mapema katika meneo ya Shayo, Kata ya Mrusi wilayani Kasulula.

Aidha Jeshi la Polisi mkoani humo, limewahakikishia usalama wa uhakika wananchi katika kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya.

Chanzo: millardayo.com