Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kutoka Mahakama Kuu, RPC Kingai anatoa ushahidi kesi ya Mbowe tena leo

Mahakamanipicdds Ushahidi wa RPC Kinondoni kesi ya kina Mbowe huu hapa

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamshna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhani Kingai ametoa ushahidi wa maelezo ya mshtakiwa wa pili Adam Kasekwa katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Kingai ametoa ushahidi huo leo Jumatano Oktoba 27, 2021 kwa hatua ya mwisho katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Ifuatayo ni ushahidi wa RPC Kingai:

Wakili: Ni wakati gani jalada la uchunguzi lilifunguliwa na wakati gani jalada la kesi

Shahidi: Jalada la uchunguzi ni mara tu baada ya kukutana na Luteni Urio alipoto taarifa ile.

Wakili: Na hili jalada la kesi

Shahidi: Ni baada ya kupata taarifa kuwa vijana waliokuwa wameelekezwa na Freeman Mbowe wamepatikana ndio nikaelekeza lifunguliwe.

Wakili: Ni taarifa gani ulikuwa nazo kabla ya kuchukua maelezo hayo.

Wakili wa utetezi Kibatala anapinga kuwa anachokifanya wakili ni kutaka kuingiza ushahidi mpya anauliza kinyume na kilichoulizwa kwenye cross examinatio

Jaji anatoa mwongozo na wakili wa Serikali anarekebisha.

Jaji anamuuliza Kibatala Kama amesikia vizuri swali naye anajibu amesikia.

Wakili Mtobesya anasema Kama shahidi akitoka nje atasema

Shahidi: Taarifa nilizokuwa nazo mimi ni taarifa kuwa Mbowe alikuwa anatafuta vijana waliofukuzwa Jeshi na walikuwa wanataka kuleta madhara kwa viongozi wa Serikali

Kwamba alikuwa na nia ya kushinikiza wananchi maandamano yasiyo na kikomo, lengo la kufanya hivyo nchi isitawalike ionekane Serikali imefeli.

Wakili: Uliulizwa jana kwamba wakati mshtakiwa wa pili Kama ulimpa onyo kuhusu taarifa ya kumtafutia ukasema ulikuwa umempa haki zake, eleza haki zake ni zipi?

Shahidi: Kumueleza kosa lake na kwamba halazimiki kusema lolote lakini atakalosema linaweza kutumika mahakamani Kama ushahidi dhidi yake

Wakili: Uliulizwa matukio yale ya kula njama yalikuwa yangefanyika Mei Mosi mpaka Agosti 2020 lakini kwenye ushahidi wako ulisema yalianza Julai kule Hotel, hebu fafanua hapa.

Shahidi: Mheshimiwa labda Kama naweza kupata hati ya mashtaka

Jaji: Kuna pingamizi utetezi kuomba hati

Mtobesy: Hakuna.

Shahidi anapewa hati na namtaka wakili aulize tena na wakili wa Serikali anarudia swali

Shahidi akisoma hati anasema wala hakuna tofauti maana hizo tarehe ziko kati ya hizo alizozitaja.

Wakili: Uliulizwa kuhusu maelezo ya mshtakiwa wa kwanza Halfani Bwirwe kuandikwa Chang'ombe ukasema nikweli na ukaulizwa kwa nini ya mshtakiwa wa pili hayakuandikwa Moshi

Shahidi: Mheshimiwa kwanza Chang'ombe Ni Dar tofauti na Moshi. Lakini pia wakati tunamkamata mshtakiwa wa kwanza hapakuwa na suala la upelelezi

Wakili Myobesya anapinga na wakili wa Serikali anarudia swali, wakati shahidi anaendelea kujibu Myobesya anasiamama akipinga kauli kuwa mshtakiwa kwanza alitudanganya akisema kuwa hilo hakulisema.

Jaji: Anakoelekea hajafika lakini neno kudanganya sikulisikia alisema aliwambia anakaa Morogoro. Jaji anaruhusu wakili wa Serikali aendelee.

Shahidi: Tulikuwa bado tunaendelea kufuatilia makazi yake maana alisema tu Temeke.

Wakili: Uliulizwa kwa nini hukumuonya kwa makosa mengine kuhusu Makosa mengine...

Kibatala anasimama na kupinga. Mimi ndio nilimuuliza maswali kuhusu chargesheet lakini sikumuuliza kwa nini.

Shahidi: Wakati naanza kuandika maelezo ya mshtakiwa nilikuwa na charge hiyo mashtaka ya kula njama hayo yaliyotokea baadaye nisingeweza kusimamisha kumhoji kwa mujibu wa charge hiyo.

Wakili: Uliulizwa kuhusu kuamini au kutokuamini sababu ya kwenda kumdhuru Sabaya, hebu eleza kwa Nini hukuamini sababu hiyo.

Shahidi: Simuamini kwamba suala la kushusha bendera (za Chadema) ndio iwe sababu ya kumdhuru lakini pia sikuamini Kama DC anaweza kwenda kushusha bendera halafu ndio sababu ya kumdhuru maana ingeleta taharuki

Wakili Kidando anaomba kielezo cha kwanza, maelezo ya mshtakiwa wa pili anampa shahidi atafute mahali ilipoandikwa baada ya kumfikisha Mheshimiwa ( Mbowe) Mikocheni ili amuulize swali.

Wakili Kidando anapekuwa maelezo kisha anampa shahidi asome sehemu hiyo na anasoma kuwa baada ya kumfikisha nyumbani mimi na Mohamed tulipewa Sh200,000 kila mmoja kujiandaa kumpokea Lissu.

Wakili: Uliulizwa kuwa hukumtaja huyo mheshimiwa ukajibu kuwa ni kweli hebu fafanua.

Mtobesya anapinga anadai kuwa tuache maelezo yajieleze si kuongeza.

Kidando anasema kuwa pingamizi halina maana

Jaji: Nafikiri pingamizi lako linakwenda kwenye thamani ya hicho anachokisema hilo Ni suala la mahakama ndio itaamua.

Shahidi anaendelea kujibu kuwa huyo Mheshimiwa ni Mbowe huku anarudi nyuma ambako mshtakiwa wa pili alishamtaja kuwa walikwenda kwake akiwa na mlinzi wake.

Wakili: Pia uliulizwa huyo Mohamed hajutajwa ni Mohamed yupi?

Shahidi: Huyu Mohamed Ni mshtakiwa wa Tau ambaye alimtaja yeye mwenyewe mshtakiwa wa pili kuwa walikuwa naye.

Wakili: Uliulizwa kuhusu kumfuatilia Sabaya Arusha na wewe ulisema hapana, hivyo naomba nikueleze sehemu hiyo kwenye maelezo

Kibatala anapinga kwanza Shahidi alishasema hapana na kwamba swali halikuwa hilo bali aliulizwa Kama walikwenda Arusha.

Jaji: Nafikiri swali halijaulizwa ameomba apewe statement na tunaomba aulize swali kwanza.

Kibatala: Mheshimiwa tunaomba tuongozwe Shahidi Kuna zoezi analifanya na dawati fulani na tumemtuma mwenzetu tunadhani anapewa information fulani ku-refresh mind

Jaji: Mimi sijaona kwa hiyo siwezi kutoa maelekezo.

Wakili wa Serikali Pius Hilla anasema wakili aache hisia na Kama Kuna kitu si cha kawaida analifanya Basi akiseme.

Jaji: Kibatala umeniomba nimuonye unasuggest kwamba Kuna taarifa za kiitelijensia siyo?

Kibatala: Si kumuona bali kutoa maelekezo.

Jaji: Nlmesema mimi sijaona hivyo siwezi kumuona na Kama Kuna kitu anataka kurefrsh jamhuru inapaswa iombe

Wakili: Eh uliulizwa pia swali kuhusiana na Kama kuna sehemu yoyote maelezo ya mshtakiwa wa pili imezungumziwa kuchukua fingerprint ukasema hakuna kwa nini hakuna?

Shahidi: Hakuna sababu hitaji la kuchukua fingerprint lilikuja baada ya kumkamata mshtakiwa wa kwanza tukaenda kumpekua tukamkuta na kijitabu chenye majina ya vituo vya mafuta na hiyo ilikua tarehe 10 Agosti lakini maelezo ya mshtakiwa wa pili nintarehe 7 Agosti

Wakili: Pia uliulizwa kuhusu fingerprint kwa mshtakiwa wa pili kwa pisto aliyokamatwa nayo, kwa nini uchunguzi huo haukufanyika

Shahidi: Mtuhumiwa aliyekamatwa na bastola alikuwa anafahamika tunachukua fingerprint pale ambapo umefanyika uvunjaji hivyo hakauwa na hitaji hilo wala DNA maana alikamatwa nayo tena mbele ya mashahidi.

Wakili: Uliulizwa ukasema hukutoa taarifa hata kwa Kamati ya ulinzi kwa nini hukutoa taarifa hizo?

Shahidi: Kwa sababu tulikuwa na uhakika na taarifa tulizokuwa nazo na kama tungezitoa kwa watu wengine tungeweza ku-create intervention isiyo ya lazima na kwa kuwa tulikuwa tunafuatilia jambo hilo kwa Siri.

Wakili: Uliulizwa pia kuhusu sheria kuruhusu mikutano na maandamano ukasena ni kweli lakini kwa kuzingatia sheria nyingine ulimaanisha Nini?

Shahidi: Ni kweli lakini lazima kuzingatia sheria nyingine maana kuan sheria nyingine kabla ya maandamano lazima upate kibali cha polisi

wakili: Sasa uliulizwa swali pia kwenye yale maelezo ya onyo kuhusu kile kifungu cha sheria ulichokiweka ukasema hiyo kasoro Ni curable, ulikuwa unamaanisha Nini?

Shahidi: Kwamba haliwezi kubadili maelezo yale Wala kuonekana kwamba hajaonywa

Wakili: Uliulizwa pia kuhusiana mshtakiwa mwingine anayeitwa Kakobe ambaye ulisema ndiye Moses Lujenge, fafanua ni wakati gani ulibaini Kakobe ndiye Kujenge.

Shahidi: Wakati tulipomkamata tulikuwa na taarifa kuwa Ni watuhumiwa watatu na tuliomuuoiza mwenzao mwingine yuko wapi akasema hajui na kwamba anaitwa Moses Lujenge

Wakili Kidando: Mheshimiwa tunaishia hapo.

Jaji: Shahidi tunakushukru kwa muda wake wote ambao tumekuwa hapa na Kama tumekukwaza basi utu umilie.

Wakili Kidando: Mheshimiwa tunaye shahidi mwingine lakini kabla ya kuendelea tunaomba ahirisho dogo tuweze kuendelea baadaye kidogo kwenye saa 5:30 Kama hakuna pingamizi kwa wenzetu.

Kibatala: Mheshimiwa jaji sisi hatuna pingamizi.

Jaji: Maombi nayakubali tunaahirisha kwa muda tutarudi mahakamani hapa saa 5:30.

Kesi imeahirishwa

Chanzo: mwananchidigital