Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusuka au kunyoa leo kesi ya walimu walioshtakiwa kumuu mwanafunzi

45054 Pic+mauaji Kusuka au kunyoa leo kesi ya walimu walioshtakiwa kumuu mwanafunzi

Wed, 6 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Bukoba. Hukumu ya walimu wawili walioshtakiwa kwa kumuua mwanafunzi wa shule ya msingi Kibeta, inasomwa leo Jumatano Machi 6, 2019 katika Mahakama Kuu, Bukoba.

Washitakiwa hao ni pamoja na Mwalimu Respicius Mtazangira na Heriet Gerald ambao walishitakiwa kwa kumuua Sperius Eradius aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo mwishoni mwa mwaka 2018.

Tayari watu wengi wamejitokeza kuja kusikiliza kesi hiyo hapa mahakamani na polisi wameimarisha ulinzi katika maeneo yote yanayozunguka mahakama hii.

Eneo la geti kuu kuingilia mahakamani hapa, kila mtu anayepita lazima akaguliwe kwanza, tofauti na hali ilivyo katika siku za kawaida.

Ndani ya ukumbi wa mahakama watuhumiwa wamekaa pande mbili tofauti wakionekana kushauriana na mawakili wao huku wakikwepa kupigwa picha na waandishi wa habari.

Walimu hao wanakabiliwa na shitaka la kuua kwa kukusudia na upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi tisa katika kesi hiyo iliyosikilizwa kwa mwezi mmoja na Jaji Lameck Mlacha, ilianza Februari 6, 2019.

Inadaiwa walimu hao walitenda kosa la kumuadhibu kwa kipigo mwanafunzi Sperius Eradius kwa madai kuwa aliiba mkoba wa mwalimu Eliet kupoteza ukiwa na fedha.



Chanzo: mwananchi.co.tz