Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kundi la ISIS laua watu Congo

ISIS Congo.jpeg ISIS

Sun, 10 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Kigaidi la ISIS limethibitisha kuhusika na shambulio katika kituo cha afya lililoua 13 wakiwemo watoto wachanga na wagonjwa huko katika mji wa Lume, Kaskazini mwa Jimbo la Kivu nchini DRC.

ISIS lilidai kupitia chaneli yake ya Telegram Jumamosi lilidai kuhusika na shambulio hilo.

Magaidi hao wanaoaminika kuwa wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF), kundi lenye silaha la Uganda ambalo limekuwa likifanya kazi katika misitu minene ya mashariki mwa Kongo kwa miongo kadhaa, walishambulia zahanati ya kanisa mwendo wa saa 10 jioni. Alhamisi, mashahidi wawili walisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live