Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kuhukumiwa kifo kisa kufanya fujo airport

HUYU NAEE.jpeg Kuhukumiwa kifo kisa kufanya fujo airport

Mon, 9 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume aliyefanya fujo katika Uwanja wa Ndege mkubwa kuliko yote nchini Thailand amekamatwa na kushtakiwa. Mojawapo ya hukumu ya makosa yake inaweza kuwa adhabu ya kifo.

Watchara Khambut (34) anakabiliwa na mashtaka 7 kutokana na tukio lililotokea tarehe 3 Mei katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Suvarnabhumi jijini Bangkok.

Kwa mujibu wa Meneja wa Uwanja huo Bw. Kittipong Kitikachon, Khambut aliwasili uwanjani hapo majira ya saa sita kasoro mchana kwa pikipiki na alijaribu kuendesha pikipiki hiyo kupitia eneo la kuchekia usalama wa wasafiri. Mara alipozuiliwa kuingia aligeuza na kuingia uwanjani humo kwa njia nyingine na kutoa bunduki.

Khambut ambaye alikutwa na bunduki feki huku akiwa ametumia dawa za kulevya,anashtakiwa kwa makosa ya kuharibu mali, kuwachanganya na kutishia kuwaumiza watu.

Sababu ya kufanya tukio hilo bado haijajulikana na mtu huyo alipoulizwa alisema kuwa haelewi ilikuwaje akafika uwanjani hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live