Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini wakidaiwa kuiba mashuka, taulo Kariakoo

Matumizipic Taulo Taulo Kortini wakidaiwa kuiba mashuka, taulo Kariakoo

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKAZI wa Dar es Salaam, Johnson Fanuel (42) na Ally Kindimba (52), wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo wakikabiliwa na mashtaka ya wizi wa mashuka, taulo na baiskeli vyenye thamani ya Sh 2,145,000 mali ya mlalamikaji, Neema Samweli.

Washtakiwa hao wamesomewa mashitaka yao jana na karani wa mahakama hiyo, Emmy Mwansasu mbele ya Hakimu Gladness Njau.

Mwansasu amedai kuwa watuhumiwa hao katika tarehe isiyofahamika kati ya mwaka 2021 na 2023 wakiwa Mkoa wa Dar es Salaam waliiba vitu hivyo kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Washitakiwa wamekana mashitaka yao na kuwekwa mahabusu hadi Julai 20, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live