Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini wakidaiwa kuiba Sh335.6 milioni za benki

Hukumu Pc Data Kortini wakidaiwa kuiba Sh335.6 milioni za benki

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: mwanachidigital

Watu wanne akiwemo mhasibu wa Benki ya I&M, Gwamaka Mboka wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la wizi wa Sh335.6 milioni mali ya benki hiyo.

Mbali na Mboka wengine ni Vicent Mwinamila (56) mfanyabiashara, Majura Mfungo (46) na Antidius Kabyemela wote ni wafanyakazi wa benki ya I&M.

Wakili wa Serikali, Aroun Titus akiwasomea washtakiwa hao hati ya mashtaka, amedai kuwa kati Septemba 6, 2019 na February 26, 2020 katika maeneo ya Dar es Salaam na Mwanza, wakiwa na nia ovu walijipatia kiasi cha zaidi ya Sh335.6 milioni; mali ya benki hiyo.

Katika shtaka la pili inadaiwa tarehe na maeneo hayo washtakiwa hao waliiba kiasi cha zaidi ya Sh335.6 milioni mali ya benki hiyo.

Titus alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema washtakiwa wana kesi ya uhujumi uchumi hivyo hawawezi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Kesi hiyo limeahirishwa hadi Oktoba 17,2023 kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: mwanachidigital