Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwakukutwa na gongo, adai ni kumtakasa mkewe..

Mbaroni Kortini kwakukutwa na gongo, adai ni kumtakasa mkewe..

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume aliyekamatwa Jumatatu Agosti 28, 2023 akiwa na lita tano za pombe haramu aina ya gongo, ameambia Mahakama ya Eldoret kwamba pombe hiyo haikuwa ya shughuli za kibiashara bali ilikuwa itumike kama dawa ya kiasili kwa tambiko la kumsafisha mkewe baada ya kujifungua pacha.

Jackson Kiprotich, ambaye amekishwa mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Eldoret Richard Odenyo, amembia mahakama kuwa bidhaa hiyo ilikuwa ya kutumika kama dawa ya kienyeji ya kumsafisha mkewe.

“Katika jamii yetu, kuzaa watoto pacha ni ishara mbaya na ili sisi kuondoa roho mbaya kwa watoto waliozaliwa, tambiko lazima lifanyike na tunatumia chang’aa kufanya sherehe ya aina hiyo,” Kiprotich amembia mahakama.

Kiprotich aliendelea kueleza mahakama kwamba lazima maafisa wa polisi waelimishwe kuhusu matambiko hayo ili kuepuka kuleta laana kwa kuzuia mila hiyo muhimu.

Ameimbia mahakama kwamba polisi wanapaswa kuelimishwa kuhusu hatari ya kuingilia mila yenye ‘uzito’ kama vile kutumia pombe kwa utakaso.

“Inasikitisha kwamba polisi hawajali umuhimu wa tambiko kama hili ambapo pombe huwa ni dawa. Serikali ingeturuhusu kuendelea kutumia pombe ya chang’aa kama dawa kama ilivyokuwa nyakati za zamani,” ameiambia mahakama.

Mahakama iliambiwa kuwa mshtakiwa alikamatwa katika kijiji cha Bunjab katika kaunti ndogo ya Moiben akiwa na lita tano za gongo kinyume cha sheria.

Amekanusha shtaka hilo na mahakama imemwachilia kwa dhamana ya KSh20,000 pesa taslimu au bondi ya kiasi sawa na hicho.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Septemba 4, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live