Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa tuhuma za kukutwa na sehemu za siri 5 za wanawake, mafuvu 2 na chuchu

Mashtaka Kisutu Nkoja.png Kortini kwa tuhuma za kukutwa na sehemu za siri 5 za wanawake, mafuvu 2 ya binadamu na chuchu

Tue, 21 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja mkazi wa Maswa, mkoani Simiyu, Salum Nkonja maarufu kama Emmanuel Nkonja, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kujibu mashtaka 11 yakiwemo kukutwa na chuchu za binadamu, sehemu za siri tano za wanawake na mafuvu mawili ya kichwa cha binadamu.

Nkonja amefikishwa mahakamani hapo leo, Juni 21, 2022 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 32/2022 na wakili wa Serikali, Caroline Materu, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa yake, Kati ya Oktoba 30, 2017 na Novemba 30, 2017 katika eneo la Ubungo lililopo Manispaa ya Ubungo.

Credit: Mwananchi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live