Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa kuwapumbaza wanawake

MBARONI.jpeg Kortini kwa kuwapumbaza wanawake

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu akiwemo mkazi wa Mlandizi, Borgas Augustino wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 16 yakiwamo ya kuwawekea dawa ya kupumbaza wanawake 10.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rohda Ngimilanga, Wakili Mwandamizi, Lucy Uisso amedai washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 16 kati ya hayo 10 ya kutumia dawa za kupumbaza wanawake, matatu ya ubakaji, mawili ya unyang'anyi wa kutumia silaha na moja la kupokea mali za wizi.

Uisso amedai katika shtaka la kwanza na la pili la unyang'anyi wa kutumia silaha linalomkabili mshtakiwa Augustino inadaiwa kati Agosti 22, 2021 na Januari 10, 2022 katika maeneo ya Sinza Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam aliiba simu tano zenye thamani ya zaidi ya Sh5 milioni na fedha taslimu Sh200, 000 mali ya Consolata Alphoce na Kanani Mustafa kabla na baada ya kuwaibia aliwatishia kwa kisu kabla.

Amedai kuwa katika shtaka la tatu hadi la 12 la kutumia dawa za kupumbaza linalomkabili mshtakiwa Augustino inadaiwa kati ya Agosti 22, 2021 hadi Februari 14, 2022 katika baadhi ya hoteli zilizopo Sinza Kinondoni pamoja na baa iliyopo Mbezi akiwa na nia ya kufanya kosa uliwapatia vidonge vya kupambaza wanawake 10.

Uisso amedai katika shtaka la 13 hadi la 15 la kubaka linalomkabili mshtakiwa Augustino inadaiwa kati ya Februari 6, 2022 kadi Februari 24,2022 ndani ya jiji Dar es Salaam akiwa na nia ovu aliwabaka wanawake watatu kwa wakati tofauti tofauti.

Alidai katika shtaka la mwisho kati ya Agosti 2021 na Februari, 2022 maeneo ya jiji la Dar es Salaam washtakiwa Augustino, Kibuga na Kondo wote kwa pamoja walipokea simu tano zenye thamani ya zaidi ya Sh14.7 milioni wakijua kuwa ni mali za wizi.

"Upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea tunaiomba mahakama hii ipange tarehe nyingine ya kutajwa," amedai Uisso

Baada ya maelezo hayo Hakimu Ngimilanga alisema mshtakiwa Augustino hatakiwi kujibu lolote kKwa kuwa anakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha na halina dhamana.

Alisema mshtakiwa Kibuga na Kondo thamana ipo wazi wanatakiwa wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh6 milioni na wawe na vitambulisho vya taifa.

Hata hivyo washtakiwa hao hawakukidhi masharti ya dhamana wamerudishwa gerezani na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 28, 2022 kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live