Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa kupiga chabo dirishani

HUKUMU Kortini kwa kupiga chabo dirishani

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKAZI wa maduka mawili Keko, Dar es Salaam, Ezra Bukasa (24) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kuingia eneo kinyemela na kuchungulia dirishani.

Mshitakiwa alisomewa mashitaka hayo jana na karani Linda Kivaju mbele ya Hakimu Gladnes Njau.

Kivaju alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Agosti 18, mwaka huu maeneo ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas) katika bweni la Kagera wilayani Ilala.

Ilidaiwa mahakamani kuwa mshitakiwa alikamatwa na mlinzi wa Suma JKT, Christopher Homoya akiwa anachungulia dirishani na baada ya kuitwa alijaribu kukimbia.

Mshitakiwa baada ya kusomewa shtaka hilo alikana kutenda kosa hilo kisha alirudishwa rumande hadi Septemba 5, mwaka huu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini atakayesaini bondi ya Sh 100,000.

Wakati huohuo, Bakari Athumani (43) alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa kosa la wizi wa Sh 210,000 na simu aina ya tecno.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live