Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa kumuua kwa risasi mfanyabiashara wa asali

Mauaji Mdf Kortini kwa kumuua kwa risasi mfanyabiashara wa asali

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu akiwemo mfanyabiashara maarufu wa asali mkazi wa Tabora mjini, Feruzi Abdallah wamepandishwa kizimbani jana Februari 2, 2023 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Wilaya ya Tabora wakituhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi mfanyabiashara ya asali, Mohammed Mustafa aliyekuwa akiishi Kata ya Mpera Manispaa ya Tabora.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa, mnamo Julai 14, 2022 majira ya saa 4.30 asubuhi huko eneo la Kazuge, Kata ya Mpera, Manispaa ya Tabora Mustafa alivamiwa na watu wawili waliokuwa wamepanda pikipiki.

Walimfuatilia wakati anatokea nyumbani kwake na walimfyatulia risasi tumboni kisha kuitupa silaha eneo la tukio na kutokomea kusikojulikana, ambapo polisi waliendelea kufanya msako na hatimaye kuwatia nguvuni watu watatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live