Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa kumiliki silaha tano na kukuta na meno ya tembo

Silaha Msmj Kortini kwa kumiliki silaha tano na kukuta na meno ya tembo

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Mashaka Mtunda mwenye miaka 32 mkazi wa Wilaya ya Sikonge amepandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka sita ambayo ni kukutwa ndani ya Hifadhi ya Pori la Uyumbu akiwa na meno mawili ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 36 pamoja na silaha tano zikiwemo bunduki aina ya shortgun na gobole.

Akisoma maelezo ya awali katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba nne (4) la mwaka 2023 mbele ya Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora, Wakili upande wa Jamhuri, Joseph Mwambwalulu alisema Mashaka Mtunda alikamatwa na askari wa TAWA ndani ya Pori hilo Januari 13, mwaka huu akiwa na meno mawili ya tembo mmoja lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 36 sambamba na kumiliki isivyo halali silaha tano na milipuko kadhaa.

Mara baada ya kuwasilishwa kwa maelezo hayo Hakimu mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Sigwa Mzige alimweleza mshtakiwa kuwa kutokana na mashtaka yanayomkabili ya uhujumu uchumi, mahakama hiyo haina uwezo kisheria kusikiliza makosa hayo ya uhujumu uchumi bila idhini ya kisheria.

Hata hivyo mshtakiwa huyo amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya masharti ya kupewa dhamana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live