Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa kukata nyaya za umeme za Sh2.3 bilioni

HUKUMU Kortini kwa kukata nyaya za umeme za Sh2.3 bilioni

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Mfanyabiashara Amos Lusekelo na mwenzake Mohamed Mbonde wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuisababishia hasara Shirika la Umeme (Tanesco) ya Sh2.3 bilioni.

Lusekelo ambaye ni mkazi wa Sinza na Mbonde, wamefikishwa mahakamani hapo leo Desemba 16, 2022, na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mary Mrio.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Sylvia Mitanto, amedai washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Akiwasomea mashtaka yao, wakili Mitanto amedai katika shitaka la kwanza, washtakiwa wanadaiwa Novemba 22, 2022 katika barabara ya Mbezi, washtakiwa waliharibu miundombinu ya Tanesco.

Wakiwa eneo hilo, washtakiwa wanadaiwa kukata nyaya zinazosambaza umeme eneo la Chang'ombe na Kiwanda cha ALAF.

Shitaka la pili, siku na eneo hilo, washtakiwa kwa kukata nyaya hizo, waliisababishia Tanesco hasara zaidi ya Sh2.32 bilioni wakati wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Hakimu Mrio amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Washitakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, Hakimu Mrio aliwaambia kuwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali Maalumu.

Upande wa mashtaka umedai, upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mrio ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 29, 2022 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.

Chanzo: Mwananchi