Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa kuiba vipande vya nondo

Hukumu Pc Data Kortini kwa kuiba vipande vya nondo

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSHTAKIWA Joshua Juma (20) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo mkoani Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka ya wizi wa vipande vya nondo.

Mshitakiwa alisomewa mashtaka yake jana na karani Caroline Nyonyi mbele ya Hakimu Gladness Njau.

Nyonyi alidai Septemba 25, 2023 huko chuo cha DIT, Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam kwa makusudi mshtakiwa aliiba vipande vya nondo 38 vyenye thamani ya Sh 60,000 mali ya Kampuni ya Shanix jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Baada ya kusomewa mashtaka yake mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo na kusomewa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja anayetambulika kisheria atakayesaini bondi ya Sh 50,000.

Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11, 2023 kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live