Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini kwa kuchomoa kitambulisho cha askari magereza

Ann Sally Nanzala Ogolla.jpeg Kortini kwa kuchomoa kitambulisho cha askari magereza kukwepa adhabu barabarani

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimamizi wa Kanisa moja la Redeemed aliyechomoa kitambulisho cha askari jela alipokamatwa kwa makosa ya kukaidi sheria za trafiki ameshtakiwa kwa kupatikana na mali ya serikali.

Ann Sally Nanzala Ogolla alishtakiwa kupatikana na kitambulisho cha mkuu wa idara ya magereza kilichopotea miaka miwili iliyopita.

Ogolla aliyejifunika shuka la Kimaasai alipatikana na kitambulisho cha Suparitenda Michael M Munyendo wa Idara ya Magereza.

Ann alikana shtaka hilo alipofikishwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani  Lucas Onyino.

Ann alishtakiwa kupatikana na mali ya Serikali kinyume na sheria nambari 324 kama inavyonukuliwa na Kifungu nambari 36 cha sheria za uhalifu.

Msimamizi huyo wa Kanisa inadaiwa alipatikana na kitambulisho hicho mnamo Februari 2, 2023 katika eneo la Westlands Nairobi. Kitambulisho hicho ni nambari  41474 cha Suparitenda Michael M Munyendo.

Kiongozi wa mashtaka Anderson Gikunda  alimweleza Onyina kwamba mshtakiwa alikamatwa na polisi wa trafiki kwa makosa ya kukaidi sheria za barabara.

Alipoitishwa kitambulisho alichomoa hicho cha idara ya magereza. Aliongezea kosa juu ya kosa.

“Naomba uniachilie kwa dhamana kwa vile mimi ni msimamizi wa kanisa na nikizuiliwa korokoroni masuala mengi kanisani yatakwama,” Ann alimsihi Bw Onyina.

Pia, aliomba apewe muda asuluhishe kesi hiyo nje ya mahakama. Bw Onyina alimwachilia kwa dhamana ya Sh40,000. Kesi imetengewa siku ya kusikilizwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live