Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini akituhumiwa kujifanya usalama, kutaka kutapeli Sh2 milioni

Takukuru Pic Data Kortini akituhumiwa kujifanya usalama, kutaka kutapeli Sh2 milioni

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kagera imemfikisha mahakamani Bruno Sella kwa tuhuma za kujifanya ofisa wa taasisi hiyo na kutaka kutapeli Sh2 milioni.

Akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo kwa miezi mitatu leo Jumanne Februari Mosi 2022 kaimu mkuu wa Takukuru Mkoa huo, Ezekia Sinkala amesema kuwa katika miaka ya hivi karibuni vimejitokeza vitendo vya baadhi ya watu wanaojipatia fedha kutoka kwa wananchi kwa njia za udanganyifu.

Amesema watu hao wamekuwa wakiwapigia simu wananchi na kujitambulisha kuwa ni maafisa wa Takukuru na kuwataka watoi fedha ili waache kuchunguza tuhuma zinazowakabili.

"Novemba 09, 2021 tapeli anayejitambulisha kwa jina la Bruno Sella alikutana na wakazi wawili wa wilaya ya Karagwe na kujitambulisha kuwa yeye ni ofisa wa Takukuru mkoa wa Kagera anayechunguza tuhuma zinazowakibili wakazi hao" amesema Sinkala

Amesema mtu huyo aliwaeleza wakazi hao ambao ni viongozi wa chama cha ushirika cha Nguvumali kuwa ili aache kuchunguza tuhuma zinazowakabili ndani ya Takukuru mkoa wa Kagera inabidi wampe Sh2 milioni.

Sinkala amebainisha kuwa baada ya kupata taarifa hiyo Takukuru ilifanya uchunguzi dhidi ya swala hilo ambapo Desemba 16, 2021 Bruno Sella alikamatwa na maafisa wa taasisi hiyo akipokea fedha hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live