Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini akidaiwa kumuingizia mtoto kidole sehemu za siri

HUKUMU Kortini akidaiwa kumuingizia mtoto kidole sehemu za siri

Wed, 19 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Nyamalembo Wilaya ya Geita, Shishi Majaliwa (47) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Geita akishtakiwa kwa kosa la kumuingizia kidole sehemu za siri mtoto wa miaka mitano kwa lengo la kujiridhisha kingono.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, Nyakato Bigirwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Verena Mathias ameeleza kuwa mstakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Juni 20, 2023.

Mathias amedai mahakamani hapo kuwa Juni 20, 2023 huko katika Mtaa wa Balenge mjini Geita mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 138C (1a) (2b) cha makosa ya kanuni ya adhabu.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kutumia vidole vyake kumsugua ukeni na sehemu ya makalio mtoto wa miaka mitano kwa lengo la kujiridhisha kingono .

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai upelelezi umekamilika na shauri limeahirishwa hadi Julai 31 litakapokuja kwa ajili ya upande wa mashtaka kusoma hoja za awali.

Aidha mshtakiwa amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na mdhamini mmoja atakaye saini hati ya Sh1 milioni pamoja na kuwa na barua ya utambulisho kutoka kwa mtendaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live