Mkazi wa Kasamwa Wilaya ya Geita, Fredy Cheyo (51) amefikishwa katika Mahakama ya wilaya hiyo akishtakiwa kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka saba.
Kesi hiyo namba 124 ya mwaka 2023 imefikishwa mahakamani leo Julai 11, 2023 mbele ya Hakimu Mkazi, Nyakato Bigirwa.
Wakili wa Serikali, Verena Mathias ameieleza Mahakama kuwa mshtakiwa huyo anadaiwa kutenda kosa la ubakaji kinyume na kifungu cha 131(1,2e na 131(3) cha makosa ya adhabu.
Mshatakiwa amekana kutenda kosa hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyomtaka kuwa na mdhamini mmoja atakaye saini hati ya Sh2 milioni, barua ya utambulisho pamoja na kitambulisho.
Kesi imeahirishwa hadi Julai 24, 2023 itakapokuja kwa ajili ya mshatakiwa kusomewa maelezo ya awali.