Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kortini akidaiwa kughushi nyaraka

Hukumu Pc Data Kortini akidaiwa kughushi nyaraka

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkazi wa Kunduchi, Thabiti Saidi (30), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka 46 yakiwemo ya kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kiasi cha Sh108.9 milioni.

Mshtakiwa huyo alisomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali, Asiath Mzamiru, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swallo, wakili huyo amefafanua mashtaka hayo akidai kuwa 23 ni ya kughushi na 23 ya kuwasilisha nyaraka za uongo

Mzamiru amedai kuwa kati ya Januari Mosi, 2022 na February 28, 2022; mshtakiwa huyo akiwa na nia ya kudanganya, alitengeza nyaraka mbalimbali za uongo zikionyesha zimetolewa tarehe tofauti tofauti na kutayarishwa na watu tofauti kutoka kampuni inayoitwa Kinglion Investment, huku wakidai fedha hizo ni kwa ajili ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi.

Amedai kuwa nyaraka hizo zilionyesha kuwa zimeandaliwa katika tarehe tofauti kati ya Januari na February zikiwa zimesainiwa na watu 23 tofauti zikionesha jumla ya Sh108.9 milioni.

Kati ya tarehe hiyo mshtakiwa huyo aliwasilisha nyaraka hizo kwa Weina katika ofisi za Wilaya ya Kinondoni, kutoka kampuni ya Kinglion Investment CO. LTD, zikionesha zinahitajika kiasi cha Sh108.9 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi huku akijua kuwa si kweli.

Katika shtaka lingine linalomkabili mshtakiwa huyo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo kati ya tarehe hizo maeneo hayo inadaiwa kuwa mshitakiwa huyo alijipatia fedha kiasi cha Sh108, 915,000 kutoka Kinglion Investment CO.LTD, akidai kuwa ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi huku akijua siyo kweli.

Hata hiyo mshtakiwa huyo amekana makosa yote yanayomkabili na upelelezi bado haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Swallo, alisema dhamana ipo wazi na amemtaka mshtakiwa awe na wadhamini wawili, watakaokuwa na hati yenye thamani ya kiasi cha fedha hizo, watatakiwa kuleta hati na uthibitisho wa mali isiyohamishika na bondi kiasi cha Sh56.5 milioni

Chanzo: www.tanzaniaweb.live