Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kondakta na abiria wanaswa wakisafirisha bangi

Bangiii Bangi

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyakazi wa Basi la Coast Line na abiria mmoja wanashikiliwa na Polisi Wilaya ya Serengeti kwa tuhuma za kusafirisha kilo 40 za bangi kutoka Tarime kwenda Arusha.

Bangi hiyo iliyokuwa imefungwa kwenye mafurushi mawili ya sandarusi yakiwa yamefichwa kwa ufundi ndani ya buti ya gari ilibainika baada ya kufanyika upekuzi wa mizigo yote ulifanyika Juni 2, majira saa 3.20 asubuhi katika kituo cha Polisi Mugumu.

Alipotafutwa kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Longinus Tibishubwamu licha ya kuita hazikupokewa,hata hivyo habari za kipolisi wilayani Serengeti zinathibitisha kukamatwa kwa Robert Mkwizu (42) mkazi wa Arusha kondakta wa basi hilo na Samwel Kenedy (34) mkazi wa kijiji cha Rung’abure Wilayani Serengeti.

Kwa mjibu wa vyanzo vyetu vya habari vinadai kuwa mapema alfajiri Juni 2, mwaka huu Kenedy alimpigia simu Kondakta Mkwizu kupakia huo mzigo katika kijiji cha Nyamwaga na kumtahadharisha kuuweka vizuri ili usikamatwe Mto Mara na kufanikiwa kupita huku yeye akipandia kijiji cha Rung’abure.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Polisi walipata taarifa kupitia vyanzo vyao vya habari kuhusiana na basi hilo kubeba madawa ya kulevya (bangi) walifuatilia na kulikamata basi hilo katika vijiji vya Matare na Nyamoko na kulipeleka Polisi kwa ajili ya upekuzi na kufanikiwa kupata kilo 40 za bangi na watuhumiwa wawili.

Sampuli imepelekwa maabara kwa ajili ya vipimo na upelelezi ukikamilika washitakiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Chacha Wangwe na Paulo Samson wakazi wa Mugumu wameupongeza uongozi wa Polisi wilaya kwa kujitahidi kudhibiti wilaya hiyo kuwa mapito ya madawa ya kulevya na kuomba wahakikishe wahusika wanachukuliwa hatua kali kwa mjibu wa sheria zilizopo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live