Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani tuhuma utakatishaji bil. 2/- za benki ya NMB

Court Kizimbani tuhuma utakatishaji bil. 2/- za benki ya NMB

Thu, 16 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKAZI 20 wa jijini Dar es Salaam wakiwamo walinzi saba wa Kampuni ya Security Group of Africa (SGA), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwamo wizi na kutakatisha zaidi ya Sh. bilioni 2 mali ya benki ya NMB.

Washtakiwa hao ni Beda Mmali (51), John Selestine (45), Kaisi Nasibu (35), Edes Hyera (43), Osward Mselema (49), Olaph Mselema (35), Manjestus Mselema (44) na wenzao 14.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Luboroga.

Wakili wa Serikali, Faraja Nguka, alidai katika tarehe tofauti mwaka 2020 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Mselema, Mwakuzi na wenzao sita walikula njama ya kuongoza genge la uhalifu ili kufanya kosa la wizi.

Ilidaiwa kwamba Juni 8, mwaka 2020 eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote waliiba Sh. 2,082,000,000 mali ya Benki ya NMB.

Ilidaiwa kwamba katika tarehe hiyo, washtakiwa hao walitakatisha kiasi hicho cha fedha wakijua ni zao la kosa la wizi.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, upande wa mashtaka ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamlika, na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa, ambapo hakimu alisema ni Julai 28, mwaka huu.

Washtakiwa wote wamerudishwa rumande kwa kuwa mashtaka ya kutakatishaji fedha hayana dhamana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live