Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa wizi wa dawa za saratani

Israel Cancer Cure 2 Kizimbani kwa wizi wa dawa za saratani

Thu, 26 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyakazi sita wa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta nchini Kenya wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na kesi ya wizi wa dawa za saratani zilizokuwa hospitalini hapo.

Nyaraka za Mahakama zilizoripotiwa na kituo cha Citizen zimewataja watuhumiwa kuwa ni Emily Nyambura, Phillip Owino, Mary Mumo, Yvonne Muthoni, Rose Jepkogei na Maureen Adongo ambao wanadaiwa kushirikiana kufanya wizi wa dawa hizo zenye thamani ya Sh.9 milioni za Kenya (sawa na Sh. 179,614,064 za Tanzania).

Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wendy Michemi watuhumiwa wote walikana mashtaka hayo. Waliachiwa kwa dhamana ya Sh. 1 Milioni ya Kenya kila mmoja.

Hakimu anayesikiliza shauri hilo aliwataka mawakili wa Serikali kuwasilisha maombi rasmi ya mashtaka baada ya watuhumiwa kupinga nyaraka zilizowasilishwa zenye mihuri ya Jeshi la Polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live