Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa tuhuma za kumkata msichana sehemu za siri kwa wembe

Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkazi wa Tandale kwa Mtogole wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam,  Siasa Samwel (30) amepandishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jana Jumatatu Agosti 19, 2019 kwa tuhuma za kumkata msichana sehemu za siri na kumsababishia maumivu.

Mbele ya hakimu Boniface Lihamwike, wakili wa Serikali,  Veronica Mtafya amedai mshtakiwa alimjeruhi msichana huyo Novemba 15, 2018 kwa kumkata sehemu za siri kwa kutumia wembe.

Mtafya amedai upelelezi wa kesi hiyo unaendelea huku mshtakiwa huyo akikana kuhusika na tukio hilo.

Wakati hakimu Lihamwike akisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa, Samwel amesema hana mdhamini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake. 

Mshtakiwa huyo alirudishwa rumande na kesi hiyo kuahirishwa hadi Septemba 2, 2019.

 

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz