Dar es Salaam. Perpetua Gondwe amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka matano ya kujipatia rushwa zaidi ya Sh16 milioni ili amtoe, Edger Fuluga katika kituo cha polisi kati, jijini Dar es Salaam.
Akisoma hati ya mashtaka jana Ijumaa Februari 21, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi, Rashid Chaungu wakili wa Takukuru, Domonic Prudence amedai kati ya Januari 18, 2020 katika kituo hicho mshtakiwa alijipatia Sh3.5 milioni kutoka kwa Scholastika Minja kwa niaba ya J1165PC, Wilbard Msaki ambaye ni mwajiliwa wa Jeshi la Polisi ili amuachie Edger Fuluga aliyekuwa anashikiliwa katika kituo hicho.
Katika shtaka la pili inadaiwa Januari 19, 2020 mshtakiwa alijipatia Sh2 milioni kutoka kwa Scholastika kwa niaba ya Msaki ili amwachie Fuluga.
Katika shtaka la tatu anadaiwa kujipatia Sh2 milioni kutoka kwa Scholastika kwa niaba ya Msaki ili amuachie Fuluga.
Shtaka la nne Januari 20, 2020 mshtakiwa huyo alijipatia Sh4.5 milioni kutoka kwa Scholastika kwa niaba ya Msaki ili amuachie Fuluga.
Ilielezwa kuwa katika shtaka la tano mshtakiwa alijipatia Sh2 milioni kutoka kwa Scholastika kwa niaba ya Msaki ili amwachie Fuluga.
Pia Soma
- Mwili wa baba mzazi wa Mtume Mwingira kuzikwa baada ya siku 30
- Magufuli kusukuma sheria bima ya afya iwe lazima
- Wabunge waliohamia CCM njiapanda
Mshtakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana na kesi kuahirishwa hadi Machi 18, 2020 itakapotajwa tena.