Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa kumnajisi mtoto wa miaka tisa

12476 PIC+KUNAJISI TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mkazi wa Kijiji cha Manyata wilayani Serengeti Mkoa wa Mara, Samwel Bugi (26) amefikishwa mahakamani leo Ijumaa Agosti 17, 2018 akishtakiwa kwa kosa la kumnajisi mtoto wa miaka tisa.

Akisoma hati ya mashtaka katika kesi ya jinai namba 204/2018; mwendesha mashtaka wa Jamhuri,  Emmanuel Zumba mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Serengeti Ismael Ngaile,  amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 14, 2018 katika Kijiji cha Manyata.

Mshtakiwa amekana shtaka na upande wa Jamhuri kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Ngaile ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 31, 2018 huku msthakiwa huyo akipelekwa rumande.

Chanzo: mwananchi.co.tz