Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa kumlawiti mtoto mwenzake

Sheria Ya Uganda Dhidi Ya Wapenzi Wa Jinsia Moja Yapingwa Mahakamani Kizimbani kwa kumlawiti mtoto mwenzake

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Watoto mkoa wa Iringa, imempandisha kizimbani Mtoto wa miaka 17, kwa shtaka la kumlawiti mwanafunzi wa miaka 13 anaesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Mwitikirwa.

Shtaka hilo limesomwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali Ahmad Magenda mbele ya Hakimu Mkazi, Edward Uphoro amesema kuwa tukio hilo limetokea November 17, 2023, katika kijiji cha Mwitikirwa, Kata ya Ifwagi, wilayani Mufindi.

Inadaiwa kuwa mtoto huyo alifanikiwa kumlawiti mwenzake walipokuwa katika msitu mnene, jambo lililofanya muathirika wa tukio hilo, kushindwa kupiga kelele kwa ajili ya kuomba msaada.

Mwendesha Mashtaka huyo amesema kuwa siku ya tukio hilo muathirika huyo alimuaga mama yake kwamba anakwenda kwa shangazi yake, na kwamba kabla hajafika alikutana na mtuhumiwa eneo la kibao cha Shule ya Msingi Mwitikirwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live