Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa kukutwa na msokoto wa bangi

Msokoto Wa Bangi Bangi Bangi Kizimbani kwa kukutwa na msokoto wa bangi

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MFANYABIASHARA Jerome Chuwa (51) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kumiliki kiasi kidogo cha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa gramu 0.87.

Chuwa alisomewa mashtaka yake jana na Wakili wa Serikali Judith Kyamba mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Amiri Msumi.

Kyamba alidai kuwa Julai 14, mwaka huu eneo la Misheni Kota Wilaya ya Ilala mshitakiwa alikutwa anamiliki pakiti moja ya bangi zenye uzito wa gramu 0.64 kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Katika mashtaka ya pili inadaiwa kuwa Julai 14, mwaka huu huko eneo la Misheni kota Wilaya ya Ilala mshitakiwa alikutwa anamiliki msokoto mmoja wa bangi wenye uzito wa gramu 0.72 kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Mshitakiwa alikana mashitaka yanayomkabili na kusomewa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja anayetambulika kisheria atakayesaini bondi ya Sh milioni moja.

Kyamba alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kusoma hoja za awali.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 9, mwaka huu kwa ajili ya hoja za awali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live