Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa kukutwa na mafuta ya Simba

Sat, 28 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Asha Sogone  maarufu Bageni mkazi wa kijiji cha Robanda amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi kwa kukutwa na nusu Lita ya mafuta ya Simba kinyume cha Sheria

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile leo ijumaa septemba 27 mwendesha mashitaka wa jamhuri Elisa Benjamini amesema mtuhumiwa alikamatwa septemba 21.2019 .

Katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba  namba 117/2019 mshitakiwa alikutwa na mafuta hayo yenye  thamani ya dola za Kimarekani 4900 sawa na sh 10,780,000.

Amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu 86(1)na(2)(c) (III) cha Sheria ya Wanyamapori namba 5/2009.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote na amelekwa mahabusu had I oktoba 7mwaka huu.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz