Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa kujifanya maofisa wa Takukuru

67069 Takukuru+pic

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa kitengo cha mauzo Hoteli ya Ramada,  William Mgatta (36) na wenzake wawili wamefikishwa katika   Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu, likiwemo la kujifanya maofisa wa Takukuru na kushawishi rushwa ya Sh300 milioni.

Mgatta na wenzake Mohammed Abdallah (25) na Daniel Ileme (35) wanakabiliwa na kesi ya jinai kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumanne Julai 16, 2019 na  kusomewa mashtaka  yao mbele ya Hakimu Mkazi, Agustina Mmbando.

Mwendesha mashitaka wa Takukuru, Aneth Mavika amedai  Mei Mosi na Juni 10, 2019 jijini Arusha wafanyabiashara Abdallah na Ileme na Mgatta walishawishi rushwa

kwa  Matunda ili wasimchukulie hatua kwa kukataa kuwalipa wafanyakazi wake Sh1 bilioni wanayomdai.

Wanadaiwa siku na tarehe tofauti katika eneo lisilotambulika jijini Dar es Salaam na Arusha, walikula njama ya kutenda kosa la kujifanya ni watumishi wa umma wakati wakijua si kweli.

Pia Soma

Katika shtaka la tatu, Juni 10, 2019 katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam na Arusha,  washtakiwa kwa pamoja walijifanya ni watumishi wa taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Washtakiwa hao walikana mashtaka yao na wakili Mavika amesema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Washtakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurejeshwa rumande na kesi kuahirishwa hadi Julai 30, 2019.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz