Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa kujifanya askari

72148 Polis+pic

Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. David Ramadhani Iddy (33) mkazi wa Tabata Segerea   amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni  kwa kosa la kujifanya ofisa wa Jeshi la Polisi na la Kujenga Taifa (JKT).

Wakili wa Serikali, Asp Hamisi amesema mbele ya hakimu, Joyce Mushi kuwa mshtakiwa anakabiliwa na makosa mawili.

Amesema Julai 19, 2019 mshtakiwa  alijifanya ofisa wa jeshi hilo na kosa la pili ni kukutwa na vifaa vya umma kinyume na sheria.

Hamisi amesema katika shtaka la kwanza mshtakiwa alijifanya ofisi wa JKT kama msimamizi msaidizi kwa kuvaa sare za jeshi hilo akijua si halali na alikutwa eneo la JKT Makao Makuu Mlalakuwa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Katika shtaka la pili, Hamisi amedai mshtakiwa alikutwa na sare za  polisi, sare moja ya kijani, nyota za vyeo mbalimbali za polisi, begi moja, kofia moja, mikanda mitatu, kofia moja ya ofisa usalama wa polisi, buti, pingu, redio call na pea moja ya sare za Tunica kinyume na sheria

Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na kudai amesingiziwa huku wakili Hamisi akieleza kuwa upelelezi  unaendelea.

Pia Soma

Mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana kwa maelezo kuwa mdhamini wake ameshindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 2, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz