Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani kwa kubaka na kumpa mimba mwanafunzi

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Paulo Nyirabu (21), mkazi wa kijiji cha Kiranero mkoani Mara amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilayani Serengeti kwa makosa mawili.

Mwendesha mashitaka wa Serikali,  Renatus Zakeo, mbele ya Hakimu Ismael Ngaile leo Jumatano Februari 13, 2019 amesema kosa la kwanza ni kubaka na la pili kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Nyamoko.

Amesema katika kesi ya jinai namba 24/2019 mshitakiwa alitenda makosa hayo Julai, 2018 tarahe isiyojulikana kwa kumbaka mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16 na kumpa ujauzito.

Mshitakiwa amekana mashtaka hayo na kurejeshwa mahabusi  hadi Februari 25, 2019 kesi utakapo tajwa tena.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz