Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani akituhumiwa kumfanyia mwenzake usaili ajira serikalini

41f9e800409caaba3e4278833a772536.jpeg Kizimbani akituhumiwa kumfanyia mwenzake usaili ajira serikalini

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VIJANA wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini mkoani Dodoma wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama kwa mmoja kwenda kumfanyia mwenzake usaili.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Senapee, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Morice Sarara kuwa Mei 8, mwaka huu katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Shule ya Informatics and Virtual Education, washtakiwa Mabula Kanga na Joel Kimatare, walifanya kosa la kuvaa uhusika wa mtu mwingine.

Sarara alidai katika shtaka la pili kuwa Mei 8, mwaka huu, Kimatare kinyume cha sheria alijitambulisha kwa Ally Mnyimwa aliyekuwa msimamizi kwamba anaitwa Mabula Edward aliyekuwa amesajiliwa kwa namba PSRS/21/3369/06 na alifanya hivyo kwa lengo la kumsaidia Mabula kufaulu usaili wa Watumishi Housing Company (WHC). Usaili huo ulikuwa ukiendeshwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Washtakiwa walikana mashtaka na wameachiwa kwa dhamana, na Mahakama iliambiwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na washtakiwa watasomewa maelezo ya awali Juni 17, mwaka huu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz