Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani akidaiwa kubaka

68155 Mahakama+pic

Thu, 25 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam . Hussen Mwinyi (23), mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaam amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la ubakaji.

Wakili wa Serikali,  Yussuf Aboud amedai leo Jumatano Julai 24, 2019 mbele ya Hakimu Mfawidhi,  Frank Mushi kuwa Juni 3, 2019 eneo la Kimara mshtakiwa alimbaka mwanamke (jina linahifadhiwa).

Wakili Aboud amedai mshtakiwa alifanya kitendo hicho bila ridhaa ya mwanamke huyo, akijua wazi kufanya hivyo ni kosa.

Mshtakiwa huyo amepata dhamana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Agosti 23, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz