Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizimbani Dar kwa madai ya kusafirisha dawa za kulevya

78145 Pic+dawa

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Geogre Mwamgabe (44), ofisa usalama wa Shirika la Posta Tanzania na dereva wa shirika hilo, Abrahamani Msimu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa  na kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin gramu 1.55 na bangi gramu 124.55.

Akisoma hati ya mashtaka leo Jumatano Oktoba 2, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,  Augustina  Mbando  wakili wa Serikali, Adolf Lema amedai  Agosti 25, 2019 makao makuu ya  shirika hilo Ilala jijini Dar es Salaam, washtakiwa  walisafirisha  bangi.

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Agosti 25, 2018 jijini Dar es Salaam walisafirisha Heroin.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hao walikana kufanya makosa hayo.

Hakimu Mmbando amesema dhamana ipo wazi lakini washtakiwa walishindwa kutimiza masharti na kurudishwa rumande hadi Oktoba 16, 2019.

Chanzo: mwananchi.co.tz