Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisena wa UDART, wenzake wafikishwa mahakamani

Kisena Dart Kisena wa UDART, wenzake wafikishwa mahakamani

Mon, 9 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo haraka, maarufu mwendokasi (Udart), Robert Kisena na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 33 yakiwemo ya kutakatisha fedha, kuongoza genge la uhalifu na kuisababishia hasara Serikali ya Sh 5.2 bilioni.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu Mei 9, 2022 na kusomewa kesi mbili tofauti za uhujumu uchumi mbele ya mahakimu wawili tofauti ambao ni Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la mawakili watano wandaamizi wa Serikali wakiongozwa na Pius Hilla akisaidiana na Jackline Nyatori, Ester Martin, Iman Mitumemingi na Upendo Temu.

Mbali na Kisena, washtakiwa wengine ni Charles Newe (48) Mkurugenzi wa Udart, mfanyabiashara John Samangu (66) na Mtunza fedha Tumaini Kulwa (44).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live