Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kisa mumewe kuchepuka, mwanamke adaiwa kumuua mtoto wa jirani na kumfukia

Kaburipic Data Kisa mumewe kuchepuka, mwanamke adaiwa kumuua mtoto wa jirani na kumfukia

Sat, 10 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia, Happyness Mkolwe (27) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Jackson Kiungo (6), mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Ihanga iliyopo mkoani hapa na kujaribu kutaka kumfukia katika shimo alilolichimba mwenyewe.

Hayo yamebainishwa jana Ijumaa, Septemba 9, 2022 na kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issah wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema siku ya tukio mwanafunzi huyo alikwenda saluni kunyoa lakini katika hali ambayo si ya kawaida, mwanamke huyo alimfuata na baada ya kumaliza kunyolewa alimchukua na kuondoka nae alikokujua mwenyewe.

Amesema alipofika huko alimsababishia kifo na kumvua nguo kisha kumfukia na baadae kumfunika na mabanzi ambayo yalikuwepo katika eneo hilo.

Kamanda Issah amesema mwanamke huyo baada ya kufanya tukio haikutosha kwani aliamua kuchimba kaburi ili amfukie mwanafunzi huyo.

“Lakini macho kuona walimuona mama huyo, hivyo hakuendelea na tukio lake hilo la kumfukia huyo mtoto ingawa tayari alikuwa ameazima vifaa kwa ajili ya kutenda tukio hilo baada ya kufuatilia tumeweza kuona vitu vya namna hiyo,” amesema Issah.

Amesema kitu cha kushangaza ni kuwa mwanamke huyo alipoulizwa aliweza kukataa katakata lakini baadae alionyesha mpaka nguo ambazo mwanafunzi huyo alivaa kabla ya kukutwa na umauti.

Amesema kisa kilichosababisha mauaji hayo kulingana na maelezo ya mwanamke huyo ni kwamba wametengana na mumewe hivyo kuna mwanamke mwingine ambaye ni mama wa mwanafunzi huyo alikuwa anakunywa pombe na mumewe hivyo alipopewa taarifa hiyo na watu wake aliamua kulipiza kisasi.

Amesema mwanamke huyo alikamatwa Septemba 8, 2022 baada ya jeshi hilo kupata taarifa kuwa Septemba 6 mwaka huu kuna mwanafunzi amepotea.

Amesema ukatili dhidi ya watoto kwenye baadhi ya maeneo mkoani Njombe upo ndiyo maana mkoa huyo ulioneka kukithiri kwa matukio hayo.

“Ndiyo maana walikuwa wanasema watoto wameuawa na watubwasiojulikana kitu ambacho si kweli bali ni mambo ya kifamilia na mtu wa karibu anayefanya mauaji hayo,” amesema Issah.

Amesema matukio yanayohusisha mauaji ya watoto wengi wao ni umri wa miaka sita kwani akivuka umri huo inakuwa bahati kwa mtoto huyo.

Amewataka wananchi mkoani Njombe kusalimisha silaha ambazo zinamilikiwa pasipo kufuata utaratibu ambao umewekwa. Amesema watakaorejesha silaha hizo kwa muda uliowekwa na serikali hakuna hatua yoyote watakayochukuliwa na jeshi hilo.

“Ila tunawasihi na kuwaambia baada ya kipindi hiki kupita tutaanza kuwasaka watu ambao wanamiliki silaha bila kufuata utaratibu,” amesema Issah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live