Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kingo za barabara zawapandisha kortini watu wanne

Thu, 4 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tabora. Watu wanne, wamefikishwa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Tabora, wakikabiliwa na makosa ya wizi, kula njama na utakatishaji fedha.

Washtakiwa hao, Mohamed Abdillah Msangi, Abdillah Mohamed, Omary Issa na Emmanuel Mtipa, wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Tabora, Sarafina Nsana leo Jumatano Julai 3, 2019.

Inadaiwa  na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Juma Masanja kuwa washtakiwa hao waliharibu miundombinu ya maeneo ya barabara ya Tabora kwenda Nzega.

Wanadaiwa kuwa walitoa kingo za barabara zinazowekwa kwa ajili ya kupunguza athari za ajali, kati ya Magiri na Ilalwansimba zenye thamani ya Sh50.6 milioni.

Shtaka la pili, wanadaiwa katika eneo la Puge kuelekea Busondo, walitoa kingo zenye thamani ya Sh62.7 milioni na eneo la tatu ni Kitangili walipotoa kingo zenye thamani ya Sh50 milioni.

Masanja amedai kuwa makosa hayo yanaangukia katika kosa la uhujumu uchumi, hivyo washtakiwa wamepelekwa rumande na shauri lao litatajwa tena Julai 15, 2019.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz