Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kingai kahitimisha ushahidi wake kesi ya Mbowe

Kingai?fit=800%2C533&ssl=1 Kingai kahitimisha ushahidi wake kesi ya Mbowe

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAMANDA wa Polisi Kinondoni, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Ramadhan Kingai amehitimisha kutoa ushahidi wake katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili kiongozi wa chama kikuu cha upinzania nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe na wenzake..

Kingai, aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Arusha, amemaliza kutoa ushahidi wake Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam leo Jumatano, tarehe 27 Oktoba 2021.

Mbele ya Jaji Joackim Tiganga, Kingai ameulizwa maswali ya mawakili wa Serikali, baada ya jana kuwa ameulizwa na mawakili wa utetezi, Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya.

Mara baada ya kumaliza, Jamhuri inakusudia kumleta shahidi mwingine kwenye kesi hiyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz