Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kina Zumaridi hawana kesi ya kujibu

ZUMARIDI Kina Zumaridi hawana kesi ya kujibu

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imesema Washtakiwa 81 kati ya 84 akiwemo Diana Bundala maarufu Zumaridi katika kesi namba 12 ya kufanya kusanyiko lisilohalali na shambulio la kudhuru mwili hawana kesi ya kujibu.

Hakimu Mkazi Mwandamizi Clescensia Mushi akisoma uamuzi huo amesema pasina shaka Mahakama imejiridhisha kwamba Washtakiwa walioachiwa huru katika kesi namba 12 hawakuguswa na vipengele muhimu vinavyotakiwa kuthibitisha makosa ya jinai.

Washtakiwa watatu kati ya 84 ndio wamekutwa na kesi ya kujibu kwa mujibu wa sheria ambao ni Juma Khamis mshtakiwa namba 05, Meshack Joseph namba 33 pamoja Daud Manyanda namba 45, ambapo Hakimu Mkazi Mwandamizi Clescensia Mushi akaihairisha kesi hiyo na itatajwa tena November 20, 2022 kwa Washtakiwa Watatu

Hata hivyo Diana Bundala maarufu Zumardi bado anakabiliwa na kesi mbili ambazo ni kesi namba 10 Shambulio la kuzuia Maafisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao na kesi namba 11 ya usafirishaji haramu wa Binadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live