Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kina Mdee watua mahakamani

Kinamdeepic Data Kina Mdee watua mahakamani

Fri, 26 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Wabunge wa viti maalum akiwemo Halima Mdee na wenzake leo Ijumaa wamefika katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuhudhuria kesi waliyoifungua mahakamani hapo ya kupinga kuvuliwa uanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mdee na wenzake wamevuliwa uanachama wa chama hicho Novemba 27, 2020 kwa sababu wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kuwapitisha.

Mbali na Mdee, wengine  ni Grace Tendega, Esther Matiko, Ester Bulaya, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Jesca Kishoa na Nusrat Hanje.

Shauri hilo bado halijaanza kusikilizwa ambapo mawakili wote wa upande wa Chadema na wa akina Mdee wameitwa kwa Jaji Cyprian Mkeha kwa ajili ya taarifa kwa ufupi.

Hali ilivyo katika Mahakama hiyo kuwa wanachama wamejitokeza kwa  wingi kwa pande zote mbili kwa akina Mdee na Chadema wakiwa wako kwenye vikundi mbalimbali

Kwa upande wa wanachama wa Chadema wamejitokeza wengi huku wengine wamevaa sare za chama.

Advertisement Wakili wa Chadema, Peter Kibatala aliwasilisha ombi mbele ya Jaji Mkeha kuwa atoe hati ya wito kwa wabunge hao ili waje kuwahoji mahakamani hapo kuhusiana na viapo vyao.

Jaji Mkeha alikubaliana na ombi hilo na kueleza hati za wito zitolewe kwa waleta maombi saba (Mdee na wenzake) kwa ajili ya kuhojiwa.

Halima Mdee, wenzake 18 wavuliwa uanachama Chadema.

Chanzo: Mwananchi