Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kina Mbowe wakutwa na kesi ya kujibu

Mbowe Kitabu Kina Mbowe wakutwa na kesi ya kujibu

Fri, 18 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imewakuta Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu na kesi ya kujibu.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaokabiliwa na kesi ya ugaidi tayari wamefikishwa Mahakamani.

Washtakiwa hao walipofika katika viwanja vya Mahakama wamelakiwa kwa shangwe na vifijo kutoka kwa wanachama na wafuasi wa Chadema na baada ya kushushwa kwenye gari wameingizwa katika mahabusu ya Mahakama kusubiri muda wa kusikiliza uamuzi.

Jaji Joachim Tiganga anayesikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ameshaingia katika ukumbi wa mahakama kwa ajili ya kutoa uamuzi imwapo washtakaiwa hao wana kesi ya kujibu ama la.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji shauri limekuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi mdogo. Sisi tuko tayari

Jaji: Utetezi?

Wakili Peter Kibatala: Nasi tupo tayari Uamuzi mdogo katika kesi ya Mbowe na wenzake unakuja chini ya kifungu 41(1) cha sheria ya uhujumu uchumi na mahakama inatakiwa kuona kama wana kesi ya kujibu ama la.

Kabla ya uamuzi huo, mahakama itapitia ushahidi wote kuona kama kuna chochote kilicholetwa cha kuwafanya washtakiwa watakiwe kujitetea.

Kama mahakama itaona wana kesi ya kujibu, itawaeleza haki zao namna ya kujitetea na kama itaona hawana kesi ya kujibu, wataachiwa huru.

Sasa hivi Jaji Joachim Tiganga anarejea mashtaka yanayowakabili washtakiwa.

Jaji: Washtakiwa wote walikana mashtaka yote, lakini walikubali taarifa zao binafsi. Mshtakiwa wa kwanza mpaka wa tatu walikiri walikuwa askari wa Jeshi Kikosi cha Makomando na waliachishwa kwa sababu za kinidhamu.

Mshtakiwa wa nne, Mbowe alikiri ni Mwenyekiti wa Chadema, lakini mengine yote walikana, hivyo ni jukumu la upande wa mashtaka kuleta ushahidi kuthibitisha mashtaka haya.

Katika juhudi za kuthibitisha, upande wa mashtaka kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha sheria ya ushahidi, waliita jumla ya mashahidi 13.

Jaji: Mashahidi walitoa vielelezo 39 yakiwemo maelezo ya onyo ya washtakiwa, bastola na risasi na maganda yake na ripoti za miamala ya fedha.

Pia walitoa taatifa za usajili wa namba za simu za wateja, hati za ukamataji mali, hati za makabidhiano ya mali zilizokamatwa kwa washtakiwa, ripoti ya uchunguzi wa kisayansi ya mawasiliano ya simu (kati ya mshtakiwa wa nne, Mbowe na shahidi wa 12, Luteni Urio), simu za washtakiwa na za shahidi wa 12.

Upande wa utetezi waliingiza vielelezo vitano yakiwemo maelezo ya mashahidi watano wa upande wa mashtaka.

Katika hatua hii, jukumu la mahakama ni kupitia ushahidi kuona kama kesi ya upande wa mashtaka imetengenezeka, ili waweze kujitetea ama la.

Jaji: Mahamama ya Rufani katikamoja ya jukumu lake kuhusu suala hilo inasema: kwa uelewa wangu katika hatua hii mahakama inatakiwa kuangalia ushahidi kwa ujumla wake na si kupima uzito na kuaminika kwa mashahidi.

Nimetumia siku mbili kupitia ushahidi wote na vielelezo vyote vya upande wa mashtaka na vya utetezi. Baada ya kupitia hayo yote haya ndio maamuzi.

Naanza na shtaka la sita kwa mshtakiwa wa kwanza, Halfani Bwire Hassan la kukutwa na mali au vifaa vya kutekelezea vitendo vya kigaidi.

Jaji: Ushahidi ulioletwa ulikuwa ni vielelezo ambavyo ni sare za jeshi na mahakama ilikataa kuvipokea kwa sababu upande wa mashtaka ulikiuka misingi ya sheria wakati waikamata vielelezo hivyo.

Hivyo mahakama inaona hawakuleta ushahidi na mahakama inatamka mshtakiwa hana kesi ya kujibu.

Kifungu namba 20 cha sheria hiyo kinaelekeza penye upungufu kurudi kwenye sheria mama, kuona nini cha kufanya.

Baada ya mahakama kurejea kifungu namba 203 cha sheria ya uendeshaji mashtaka, kinachoeleza kama washtakiwa wanakiri ya kujibu itatamka wanaachiwa huru.

Hivyo mahakama inatamka kuwa mshtakiwa wa kwanza hana kesi ya kujibu na anaachiwa huru.

Mashtaka mengine mahakama imefanya uchunguzi imeona kwamba upo ushahidi ambao umeleta tuhumua kiasi cha kufanya kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu katika shtaka la kwanza hadi la tano.

Hivyo mahakama inaelekeza kuwa wanaweza kuleta utetezi wao na hata kuleta mashahidi au kukaa kimya.

Wakijitetea kwa kiapo, upande wa mashtaka utawahoji na wakikaa kimya, basi mahakama itaweza kuamua. Hivyo, mahamama inawaalika washtakiwa waeleze ni kwa namna gani wataleta utetezi wao.

Wakili Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji tumepokea uamuzi ya mahakama kwamba mshtakiwa wa kwanza ana kesi ya kujibu kwenye kosa la kwanza, la pili na la nne, amenieleza atajitetea mwenyewe chini ya kiapo na anategemea kuita mashahidi wengine watano, hivyo yeye atakuwa ni wa sita.

Pia amenieleza katika kuleta utetezi atatoa vielelezo vitano. Wakili John Mallya; Mshtakiwa wa pili, Adamu Kasekwa kwa makosa aliyopatikana na kesi ya kujibu matatu ataleta ushahidi wake chini ya kiapo na mashahidi wawili pamoja na vielelezo vine.

Wakili Fredrick Kihwelu: Mshtakiwa wa tatu, Mohamed Ling'wenya atajitetea chini ya kiapo, atakuwa na mashshidi watano pamoja na vielelezo vitano: Wakili Peter Kibatala; Mshtakiwa wa nne, Mbowe atajitetea kwa kiapo, ataleta mashshidi 10 na yeye wa 11 na ataleta vielelezo 20.

Baada ya hapa nafahamu kuwa mtanitaji nakala ya proceedings Wakili wa Serikali Kidando: Mheshimiwa Jaji tulikuwa tunapitia Rule 15 (2) za Ecomonic procedure na inatakiwa pande zote mbili zitoe majina na anuani ya mashahidi pamoja na vielelezo.

Wakati wa usikilizwaji waliorodhesha mashahidi wane, lakini wakaomba wasi-desclose majina ya mashahidi wengine, sasa wanatakiwa waweke wazi.

Wakili wa Serikali Kidando: Hivyo tunaomba wenzetu wacomply hiyo kanuni kwa kutoa idadi na majina ya mashahidi na anuani zao na vielelezo ambavyo watavitumia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live