Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilo 11 za dawa za kulevya zanaswa kwenye 'wheel chair'

M Kiti Kilo 11 za dawa za kulevya zanaswa kwenye 'wheel chair'

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong wamepata kilo 11 za dawa inayoshukiwa kuwa ya Cocaine ikiwa imefichwa kwenye kiti cha magurudumu cha umeme.

Dawa hiyo yenye thamani ya dola milioni 1.5, ilipatikana wakati mwanamume mwenye umri wa miaka 51 alipokuwa akifanyiwa ukaguzi wa forodha siku ya Jumamosi.

Mwanamume huyo, ambaye aliwasili kutoka nchi ya kisiwa cha Caribbean ya Sint Maarten kupitia mjini Paris siku ya Jumamosi, amekamatwa.

Anaweza kukabiliwa na kifungo cha maisha jela iwapo atapatikana na hatia ya kusafirisha dawa hatari za kulevya.

Kulingana na maafisa wa forodha, mshukiwa alileta kiti cha magurudumu kama moja ya mizigo miwili iliyokaguliwa.

Uchunguzi zaidi uliamriwa wakati wafanyikazi walipotilia shaka na wakapata ushahidi kwamba mto wa kiti ulikuwa umeshonwa tena.

Mwanamume huyo, ambaye sio mkazi wa Hong Kong na anayekabiliwa na changamoto ya uhamaji, inasemekana aliwaambia maafisa kuwa yeye ni mkurugenzi wa kampuni ya kukodisha magari na kwamba aliazimwa kiti hicho cha magurudumu na rafiki yake. Uchunguzi wa tukio hilo umeanzishwa.

Maafisa wa forodha walisema katika hatua ya kukabiliana na visa kama hivyo wataimarisha ukaguzi kwa wageni kutoka "maeneo hatarishi" ili kukabiliana na shughuli za kimataifa za usafirishaji wa dawa za kulevya. Takriban watu 178 walikamatwa kuhusiana na visa kama hivyo mwaka jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live