Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilo 100 za bangi zamtupa jela miaka 25

Msokoto Wa Bangi Bangi Bangi Kilo 100 za bangi zamtupa jela miaka 25

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro imemhukumu kifungo cha miaka 25 jela, John Mwasikili baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi, zenye uzito wa kilo 107.29.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji M.P. Otaru amesema ushahidi uliotolewa na mashahidi 16 na vielelezo 15 vya upande wa mashtaka haukuacha shaka dhidi ya mshtakiwa kutenda kosa hilo.

Mahakama iliambiwa kwamba bangi aliyokuwa nayo :mfungwa huyo mpya' ilikuwa kwenye mifuko nane maarufu sulphate, katika gari aina ya Toyota Kluger, yenye namba za usajili T 895 CQR.

Mahakama pia imeamuru gari hilo lenye namba T 895 CQR litaifishwe na kielelezo, kwa maana ya hiyo bangi iteketezwe.

Mwasikili alikamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Machi 15, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live