Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichotokea kesi ya kigogo wa Takukuru hiki hapa

74545 Kigogo+pic

Sat, 7 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upelelezi katika kesi ya kuomba na kupokea rushwa inayomkabili, Mchunguzi Mkuu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa(Takukuru), Cosmas Batanyita( 44), bado haujakamilika.

Batanyita anakabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kuomba rushwa ya Sh200 milioni na kutakatisha fedha.

Leo Ijumaa Septemba 6, 2019 Wakili wa Serikali Tully Helela ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Helela amedai mbele ya hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mwaikambo ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 20, 2019 kesi hiyo itakapotajwa.

Mshtakiwa amerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

Batanyita amefikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza, Agosti 9, 2019 na kusomewa kesi ya uhujumu uchumi namba 76/2019

Kati ya mashtaka hayo saba; mashtaka matatu ni ya kushawishi rushwa, moja la kuomba na kupokea rushwa na mashtaka matatu ni ya kutakatisha fedha.

Baadhi ya mashtaka yanayomkabili Batanyita, anadaiwa Februari 9, 2019 katika eneo la Upanga, Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alishawishi na kuomba rushwa ya Sh200 milioni kutoka kwa Hussein Gulamal Hasham ili aweze kuharibu ushahidi katika kesi ya ukwepaji wa kodi ilivyokuwa inamkabili Hasham, wakati akijua  kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa unaendelea katika Ofisi ya Takukuru.

Pia, anadaiwa kuwa Februari 10, 2019 katika eneo la Sabasaba, Batanyita alijipatia dola za kimarekani (USD) 20,000 kutoka Faizal Hasham ili ikiwa ni ahadi ya kuharibu ushahidi katika kesi ya ukwepaji kodi inayomkabili Hussein Hasham, wakati akijua upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa unaendelea.

Vile vile, Februari 13, 2019, katika ofisi ndogo za Takukuru zilizopo Masaki, mshtakiwa alishawishi rushwa ya dola za kimarekani (USD) 50,000 kutoka kwa Thangvelu Vall, kama ahadi ya kuharibu ushahidi katika kesi ya kukwepa kodi inayomkabili Vall.

Katika shtaka la kutakatisha fedha, Batanyita anadaiwa Februari 19, 2019 eneo la Chamazi, akiwa mwajiri wa Takukuru, alitumia fedha alizopewa kwa njia ya rushwa, kununulia kiwanja eneo la Chamazi, kwa gharama ya Sh15,8000,000, wakati akijua fedha hizo ni zao tangulizi la kosa la kuomba rushwa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz