Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichokwamisha kesi ya wafuasi Chadema hiki hapa

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upande wa mashtaka katika kesi ya kufanya mkusanyiko usio halali inayowakabili washtakiwa 31 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaita wadhamini wa washtakiwa waliokaidi kufika mahakamani.

Wakili wa Serikali, Elia Atanas amedai leo Jumanne Juni 4,2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Agustin Ruizile kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya washtakiwa kuwasomea maelezo ya awali (PH) lakini wengi wao hawapo mahakamani.

"Kwa mujibu wa sheria mshtakiwa anaposomewa maelezo ya awali anatakiwa kuwapo mwenyewe mahakamani ili aweze kujibu hoja atakazosomewa" amedai Atanas

Wakili Atanas pia ameiomba Mahakama kuwaita wadhamini wa washtakiwa wote waliokaidi kufika mahakamani ili waje kueleza sababu za wao kukaidi amri ya Mahakama.

Wakili wa utetezi Alex Massaba akisaidiana na Hekima Mwasipu wamedai  wako tayari kuendelea na kesi hiyo kwa kuwawakilisha washtakiwa 15 waliofika mahakamani.

"Historia ya kesi hii washtakiwa hawajawahi kutimia hata mara moja tunaomba Mahakama iendelee kwa kuwasomea maelezo ya awali kwa washtakiwa waliopo na ambao hawapo mahakama itoe uamuzi," amedai Mwasipu.

Pia Soma

Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 3, 2019 na kuwataka washtakiwa wote kuwepo kwaajili ya kuwasomea hoja za awali.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya jinai namba 51 ya  mwaka 2018,  ni Thabita Mkude, Haji Lukwambe, Emmanuel Kimoi, Mohammed Juma, Hussein Mrombo, Abdallah Hamis, Hussein Kidda, Paulo Kimoro, Brayan Morris, Hussein Nguli na Edna Kimoro.

 

Wengine ni  Jonathan Lema, Salha Ngondo, Ramadhan Mombo, Godwin Mwakasungura, Hassan Kibweda, Omary Hamad, Fatima Ramadhan, Ezekiel Nyenyembe, Denis Mtegwa, Dickson Kerefu, Raphael Mwaipopo, Athuman Mkawa, Mussa Kusigila.

Pia wamo,  Omary Danga, Jackson Masilingi, Asha Kileta, Ally Rajabu,  Isack Ng'aga, Erick John na Aida Olomi.

Kwa pamoja wanadaiwa Februari 16,  2018 huko Kinondoni jijini Dar es Salaam katika eneo la Mkwajuni, Wilaya ya Kinondoni walifanya mkusanyiko usio wa halali na kinyume cha sheria.

Ilidaiwa mkusanyiko huo ulikuwa na nia yakufanya uvunjifu wa amani na kusababisha taharuki  kwa wananchi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz