Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichokwamisha kesi ya kigogo Takukuru chabainishwa

61344 Pic+takukuru

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar ss Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imetuma maombi nje ya nchi kwa ajili ya kufanya upelelezi katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili, aliyekuwa mkurugenzi wa mipango na ufuatiliaji na tathmini wa Taasisi hiyo, Kulthum Mansoor.

Mansoor anakabiliwa na makosa nane likiwemo la utakatishaji fedha kiasi cha Sh1.4 bilion, katika kesi ya uhujumu uchumi, iliyopo  mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Takukuru, Maghela Ndimbo ameieleza Mahakama hiyo leo Jumanne, Juni 4, 2019, mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina.

Ndimbo amedia kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika.

"Tumetuma maombi nje ya nchi kwa ajili ya kukamilisha upelelezi katika nchi hizo, hivyo tunasubiri majibu kuhusiana na maombi hayo," amedai Ndimbo.

Ndimbo baada ya kueleza hayo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 18, 2019 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa  rumande kutokana na mashtaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

Pia Soma

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa anadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 akiwa Makao Makuu ya Takukuru iliyopo jijini Dar es Salaam, alighushi na kutoa  barua ya ofa ikionyesha barua hiyo imetoka katika halmashauri ya Bagamoyo huku akifahamu kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Kuanzia shtaka la pili hadi la saba, anadaiwa, kati ya Januari 2012 na Mei 2017 akiwa eneo la Upanga, mshtakiwa alijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh1.477,243,000 kutoka kwa watumishi  sita wa Takukuru, kama malipo ya viwanja vilichopo kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo huku akionyesha yeye ni mmiliki, jambo ambalo alijua ni uongo.

Katika kosa la nane, ambalo ni la kutakatisha fedha, mshtakiwa anadaiwa  kati ya 2013 na Mei 2018 akiwa eneo la Upanga jijini Dar es Salaam, alijipatia  kiasi hicho cha fedha huku akijua fedha hizo ni zao la makosa mengine.

Chanzo: mwananchi.co.tz