Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kilichokwamisha kesi ya Kisena, wenzake chabainishwa

72991 KISENAPIC

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kesi ya utakatishaji wa fedha inayomkabili, Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka, maarufu Mwendokasi (Udart), Robert Kisena na wenzake imeshindwa kuendelea kutokana na Hakimu anayeendesha shauri hilo hayupo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu Agosti 26,2019 kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa lakini Hakimu anayeendesha shauri hilo hayupo.

"Kuna jambo tulipanga tuliongelee leo kwa kuwa hakimu anayeendesha shauri hili hayupo naomba ipangwe tarehe nyingine," alidai Simon.

Shauri hilo limeahirishwa hadi Septemba 4, 2019 litakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 38/2019 ni mke wa Kisena, Florence Mashauri; Kulwa Kisena; raia wa China, Chen Shi na Mhasibu wa Kampuni hiyo, Charles Selemani Newe.

Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa kati ya Januari Mosi, 2011 na Mei 31,2018 ndani ya jiji la Dar es Salaam, waliongoza genge la uhalifu.

Pia Soma

Katika shtaka la pili, linawakabili washitakiwa wanne ambao ni Kisena, Kulwa, Simon na Florence ambalo ni kujenga kituo cha mafuta ya petroli bila kibali kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura).

Wanadaiwa kutenda kosa hilo Januari Mosi mwaka 2015 na Desemba 31, 2017 ambapo inadaiwa walijenga kituo hicho eneo la Jangwani bila kibali cha Ewura

Katika shtaka la tatu, washitakiwa hao inadaiwa kwa kipindi hicho wakiwa wakurugenzi walifanya biashara eneo ambalo halijaruhusiwa kujengwa.

Pia, katika shitaka la nne inadaiwa waliiba Sh1.2 bilioni mali ya Udart huku mashtaka manne ni utakatishaji wa fedha.

Kisena, mkewe walivyoachiwa huru kisha kushtakiwa upya

Mengine ni mashtaka manne ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo; manne ya wizi; moja kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja ni kusababisha hasara Udart.

Kisena wa Udart, wenzake wafutiwa mashtaka

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz